Bodi ya ligi imethibitisha kuwa kesho Ijumaa watamtangaza Mdhamini wa ligi kuu msimu huu baada ya kukamilisha mazungumzo
Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Boniface Wambura amesema Mdhamini atajulikana kesho
"Kesho tutamtangaza mdhamini mkuu wa ligi kuu kuhusu tukio hilo litafanyikia wapi na saa ngapi tutatoa mwaliko rasmi muda wowote kutoka sasa," amesema Wambura
Licha ya jambo hilo kufanywa kwa usiri, inaelezwa Kampuni ya Vodacom inarejea rasmi kuidhamini ligi baada ya makubaliano mapya kufikiwa baina yake ya TFF
Moja ya sababu zilizopelekea Vodacom kujitoa msimu uliopita ni suala la ongezeko la timu kutoka 16 mpaka 20
Tayari TFF imekubali kupunguza idadi ya timu ambapo msimu wa 2020/21 ligi itakuwa na timu 18 kisha kupungua zaidi msimu utakaofuata kubaki 16
No comments:
Post a Comment