Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta usiku wa Ijumaa ya August 23 2019 atakuwa katika uwanja wao wa nyumbani Luminus wakicheza dhidi ya Anderlech ya Ubelgiji katika mchezo wao wa tano wa Ligi Kuu Ubelgiji.
Samatta kwa mara ya kwanza atakuwa anakutana na nahodha wa zamani wa Man City Vincent Kompany ambaye atakuwa katika safu ya ulinzi ya Anderletch wakati ambao Samatta akipambana kutia nyavu, Kompany ambaye ni kocha mchezaji wa Anderletch anaingia katika mchezo huo akiwa na rekodi mbovu wakati Samatta anaingia akiwa wa moto baada ya kutoka kufunga hat-trick.
Kuelekea mchezo huo baada ya kuwa na matokeo mabovu kwa Anderletch katika mechi zao nne za mwanzo wakifungwa mbili na kutoa sare mbili, Vincent Kompany ameamua kutangaza rasmi kuwa hatokuwa kocha katika siku ya mechi na amejipa unahodha, huku Simon Davies akimtangaza kama ndio atakuwa kocha mkuu wa mechi, Genk wapo nafasi ya 8, wameshinda game 2 na kupoteza mbili wakati Anderletch wapo nafasi ya 13 katika msimamo wenye timu 16.
No comments:
Post a Comment