Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, KMC wameyaaga mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa AS Kigali ya Rwanda
AS Kigali walijipatia mabao yao kwenye kila kipindi yakiwekwa kimiani na Rashid Kalisa na Eric Nsabimana
Bao pekee la KMC lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Yusuf Ndikumana kwenye dakika ya 86
Licha ya kupata matokeo ya suluhu ya bila kufungana ugenini, KMC imeshinda kutumia vyema uwanja wa nyumbani
No comments:
Post a Comment