Baada ya KMC kupoteza mchezo nyumbani jana kwa kufungwa mabao 2-1 na AS Kigali na kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, msemaji wa Simba Haji Manara amesema matokeo hayo yanapaswa kuwa somo kwao na wasiwadharau wapinzani wao UD Songo
Simba itashuka kwenye uwanja wa Taifa kesho Jumapili kuikabili UD Songo katika mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika
Timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Msumbiji
Manara amesema matokeo ya KMC jana yamewaumiza mashabiki wote wazalendo ambao wangependa kuona timu zote za Tanzania zinafanya vizuri kwenye michuano ya CAF
"Ni kweli inauma kwenu na kwa Watanzania wote lakini nyinyi ni mashujaa kamili,msimu wenu wa kwanza kuja kucheza michuano mikubwa kama hii ,hakika mnalo la kujivunia," amesema
"Na kwetu Simba hii ina maana kubwa sana,tusijiamini kupita kiasi,bado hatujafuzu hadi tushinde baada ya dakika tisini"
"Wachezaji na benchi la ufundi wajue hilo na sote kila mmoja kwa nafasi yake atambue hilo"
"Twendeni Kwenye vita kamili ya dakika tisini za Jasho na Damu,Washabiki mtimize wajibu wenu kwelikweli kwa kuhanikiza mwanzo mwisho"
No comments:
Post a Comment