Mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga leo wamefanikiwa kuilaza AFC Leopards kutoka Kenya kwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Mchezo huo wa maandalizi ya mwisho kabla ya Yanga kusafiri kuifuata Township Rollers, uliishudia Yanga ikiwa bora katika kujilinda na kutengeneza mashambulizi
Ulikuwa ni mchezo wenye matumizi makubwa ya nguvu, wachezaji wa Yanga wakionyesha kuimarika kimwili, wameonyesha kuwa fit kwelikweli
Pamoja na kosakosa za hapa na pale, Yanga ililazimika kusubiri hadi dakika ya 84 kupata bao lake la ushindi likiwekwa kimiani na Papy Tshishimbi
Tshishimbi aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Patrick Sibomana
Kikosi cha Yanga kilichocheza leo kimeonyesha utofauti mkubwa na kile kilichofungwa mabao 2-0 na Polisi Tanzania juzi
Hakika wachezaji wa kikosi hiki wanastahili kuitwa kikosi cha kwanza
Yanga inatarajiwa kurejea mkoani Kilimanjaro ambako itaondoka siku ya Jumanne kuelekea Afrika Kusini
No comments:
Post a Comment