Kiungo Shariff Elden Shiboub juzi aliibuka nyota wa mchezo akiifungia Simba mabao kwenye ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Azam Fc
Kiungo huyo aliyetua Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Al Hilal ya Sudan, kwa sasa ndio habari ya mjini kutokana na umahiri wake anaoonyesha dimbani
Shiboub amesema mabao yake aliyofunga kwenye mchezo huo ni mwanzo tu, mambo mazuri mengi yanakuja Msimbazi
"Tunawashukuru mashabiki wetu kwa kuendelea kutuunga mkono, wao ni chachu ya mafanikio tunayopata"
"Huu ni mwanzo tu, watarajie mambo makubwa zaidi kutoka kwangu," alisema Shiboub
Kwenye mchezo dhidi ya Azam, Shiboub alionyesha umahiri mkubwa katika kushambulia na hata kwenye ulinzi
No comments:
Post a Comment