Mtu mmoja anayetajwa kuwa Injinia wa Meli ya MV Mapinduzi inayofanya safari zake Unguja na Pemba, Haji Abdallah Khatib, amejinyonga wakati Meli hiyo ikiwa safarini kutoka Unguja kwenda Pemba.
Mkurugenzi wa Shirika la Meli na Uwakala Zanzibar Salum Ahmada Vuai, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo ameeleza kuwa mtu huyo alikuwa kwenye chumba cha mashine na alikuwa peke yake.
''NI kweli amejinyonga lakini ni mapema sana kujua chanzo lakini Meli imelazimika kukatisha safari yake na kurejea Unguja kwaajili ya uchunguzi zaidi'', amesema Vuai.
Awali Kamanda wa Polisi wa Mjini Magharibi Thobias Sedeyoka, alisema kuwa athari ya tukio hilo inakwenda kwa abiria wengine ambao leo ni siku ya kwanza ya wiki na walikuwa wanakwenda kwenye majukumu yao lakini wanalazimika kurudi.
''Bado tunaongea na mamlaka husika ili kujua lakini tu kama mnavyofahamu leo ni Jumatatu watu wanakwenda kwenye shughuli zao huo Pemba lakini sasa wanarudi Unguja ili tuupate mwili na tufanye uchunguzi kisha tutawajulisha zaidi'', ameeleza.
No comments:
Post a Comment