Leo Yanga ilicheza mchezo wa tatu wa kirafiki dhidi ya ATN Academy mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya
Kwa mara nyingine, Yanga imetoa dozi ya mabao 7-0 huku Patrick Sibomana na Sadney Urikhob walikufanga mabao matano, Sibomana matatu na Sadney akipachika mabao mawili
Mabao mengine mawili yalifungwa na Juma Balinya na Lamine Moro
Awali Yanga ilipaswa kusafiri mkoani Dodoma kucheza na Dodoma Fc, lakini maadiliko yaliyofanywa na uongozi wa timu hiyo yameipa ATN Academy nafasi ya kumenyana na mabingwa hao wa kihistoria
Kikosi cha Yanga kilichoanza mchezo huo;
Kabwili, Ally Ally, Marcelo, Lamine, Mustapha,Banka, Balama, Tshishimbi, Sadney, Balinya, Sibomana
No comments:
Post a Comment