Droo ya hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika imefanyika leo nchini Misri ambapo kwa mara ya pili Yanga imepangwa kucheza na Township Rollers ya Botswana
Mwaka jana Yanga ilikutana na Rollers kwenye raundi ya kwanza na ikaondoshwa katika michuano hiyo kwa kuchapwa mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Mchezo wa marudiano uliopigwa Botwasana, tmu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana
Yanga itaanzia jijini Dar es salaam ambapo mchezo wa kwanza utapigwa uwanja wa Taifa kati ya August 09-11
Mchezo wa marudiano utapigwa kati ya August 23-25 nchini Botswana
No comments:
Post a Comment