We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, July 24, 2019

Waziri azindua kiwanda cha makaravati ya plastiki

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, leo Julai 24 amezindua kiwanda kinachotumia teknolojia mpya ya utengenezaji wa makaravati kwa kutumia plastiki.
Kiwanda hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam kitakuwa ni cha pili barani Afrika, baada ya kiwanda kilichopo Afrika Kusini kuwa na teknolojia hiyo ya kutumia plastiki kutengeneza makaravati.
Akizungumza baada ya uzinduzi wa kiwanda hicho, Waziri Bashungwa amesema kuwa kiwanda hicho kinatumia teknolojia ya kisasa ya nchini Finland, ambapo kitakuwa ni cha kwanza Afrika Mashariki kikiwa na uwezo wa kutengeneza mabomba ya maji taka, mabomba ya maji safi pamoja na mabomba ya makaravati ambayo yatakuwa mbadala wa makaravati ya zege au mabati.
"Kiwanda hiki ni 'heavy weight' na ninafurahi kwamba malengo ya serikali kuvutia uwekezaji Tanzania lakini kwa kutazama soko la Afrika Mashariki na SADC, ninawapongeza Plasco kwa kuunga mkono jitihada za serikali", amesema Bashungwa.
Aidha Waziri Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi wa Shirika la viwango Tanzania TBS kufika mara moja katika kiwanda cha Plasco na kufanya mazungumzo ya namna gani ataweza kuwapa ithibati ya bidhaa zao kukubalika na kupata soko kiurahisi ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list