Klabu ya Simba huenda ikaingiza zaidi ya Mil 150 kama itakubali kumuuza kiungo wake Mzamiru Yassini ambaye anawaniwa na timu ya Haras El Hadad kutoka nchini Misri
El Hadad inayoshiriki ligi kuu ya Misri, imeonyesha nia ya kutaka kumsajili Mzamiru ambapo taarifa zimebainisha kuwa imewasilisha ofa ya dola 70,000 (zaidi ya Mil 150)
Inaelezwa mabosi wa Simba wako katika mazungumzo ya mwisho na klabu hiyo na wanaweza kumruhusu Mzamiru akajaribu bahati yake huko Misri
Ujio wa Francis Kahata, Ibrahim Ajib na Sharaff Shiboub umeimarisha safu ya kiungo ya Simba ambayo pia itaendelea kuwa na Jonas Mkude, Hassani Dilunga na Said Ndemla bila kumsahau kiraka Erasto Nyoni
Hivyo hata kama wataamua kumuuza Mzamiru, Simba haitaathirika
Timu za Misri zimeonekana kuvutiwa na nyota wa Simba kwani kama dili la Mzamiru litakamilika, atakuwa mchezaji wa pili kuuzwa huko Misri mwaka huu baada ya Shiza Kichuya
Usajili wa Kichuya kwenda klabu ya ENPPI uliingizia Simba Milioni 200
No comments:
Post a Comment