Uwezekano wa Real Madrid kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba, 26, utategemea kuondoka kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 30, kuondoka klabu hiyo ya Uhispania. (AS)
Bale, ambaye anapokea pauni 550,000 kwa wiki katika uga wa Bernabeu, ambako ana mkataba wa hadi mwaka 2022, anataka marupu rupu yanayolingana na wachezaji wakuu duniani kuondoka Real Madrid, kinasema chanzo cha habari kilicho na uhusiano wa karibu na nyota huyo. (Sky Sports)
Barcelona wako tayari kufanya mazungumzo na Lionel Messi, 32, kurefusha mkataba wa nyota huyo raia wa Argentina kwa miaka minne zaidi. (ESPN)
Tottenham wanajiandaa kutumia tena kitita kikubwa cha fedha wiki hii kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Real Betis na Argentina Giovani lo Celso, 23, pamoja na mlinzi wa wa chini ya miaka 21 wa Fulham na England, Ryan Sessegnon, 19. (Mirror)
Fulham wanataka pauni milioni 40 kumuachilia Sessegnon lakini Spurs wanamini wanaweza kuafikiana kwa mkataba wa karibu pauni milioni 25 kumnasa mchezaji huyo ambaye amesalia na mwaka mmoja kukamilisha mkataba wake Craven Cottage.
Sessegnon pia anapania kusalia London, japo vilabu vingine vikubwa kama vile Manchester United, Paris St-Germain, Juventus na Borussia Dortmund pia vimekuwa vikimfuatilia. (London Evening Standard)
Toby Alderweireld anatarajia kubaka Tottenham, licha ya Roma kuhusishwa na uhamisho wa mlinzi huyo wa miaka 30 raia wa Ubelgiji ambaye masharti ya mkataba wake yanasema lazima auzwe ikiwa klabu inayotaka kumnunua ina uwezo wa kufikia ada ya pauni milioni 25 kufikia Alhamisi wiki hii. (Telegraph)
Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri anataka kumjumuisha mlinzi wa Tottenham Danny Rose, 29, katika kikosi chake cha Juventus. (Mail)
Atletico Madrid huenda wakaelekeza juhudi zao katika harakati ya kumsaka mchezaji nyota wa Real Madrid MColombia James Rodriguez, 28, badala ya kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27. (Marca)
Antoine Griezmann, 28, ameashiria kuna ''uwezekano'' wa kujiunga na Manchester United siku zijazo huku mchezaji huyo mpya wa Barcelona akielezea azma yake ya kucheza na mchezaji mwenza wa Ufaransa na mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 28, katika soka ya kiwango cha vilabu. (Goal.com)
Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, anajiandaa kutia saini mkataba ulioboreshwa wa thamani ya pauni milioni 117 ambao huenda ukaendelea hadi mwaka 2025, na pia anataka kuwa nahodha Old Trafford. (Manchester Evening News)
Mlinzi wa England Harry Maguire, 26, hana mpango wa kuhama Leicester licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa Manchester United. (Leicester Mercury)
Juventus wako tayari kuizia Manchester United mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, msimu huu wa joto, bei yao ya kati ya £70m na pauni milioni 90 ikifikiwa. (Mail)
Mshambuliaji wa zamani wa Crystal Palace Clinton Morrison anatarajia mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, atasalia katika uwanja wa Selhurst Park msimu huu, licha ya mchezaji huyo kunyatiwa na Arsenal Bayern Munich. (Talksport)
Arsenal wako mbali sana kufikia kiwango cha pauni milioni 80 zinazoitishwa na Crystal Palace kumwachilia Zaha, huku wasimamizi wa Selhurst Park wakipuuzilia mbali ofa za hivi karibuni za kutaka kumnunua kiungo huyo. (Independent)
Wolves wako tayari kuweka dau la pili la kumnunu a mlinzi wa Olympiacos Pape Abou Cisse, 23. (Sport Witness, via Birmingham Mail)
Kiungo wa kati wa Brighton Taylor Richards, 18, anasema haikuwa rahisi kufanya uamuzi wa kuondoka Manchester City kwenda Seagulls. (Argus)
Tetesi Bora Jumatatu
Klabu ya ligi ya Uchina Beijing Guoan wamepania kumsajili winga wa Real Madrid Gareth Bale. Klabu hiyo, ina mpango wa kumfanya winga huyo mwenye miaka 30 kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi ya Uchina. (telegraph)
Manchester United, ambao awali walikuwa wakimnyemelea Bale wamejitoa katika mbio za kumsajili mchezaji huyo. (Manchester Evening News).
Beki wa Arsenal na Ufaransa Laurent Kolscielny amekubali kujiunga na klabu ya Rennes.
Arsenal inatarajiwa kuishinda Tottenham katika kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos. Mchezaji huyo wa Uhispania atajiunga kwa mkopo.(Mirror)
Kiungo wa kati wa Liverpool na Uingereza James Milner ,33, amesema hajui hatma yake katika klabu hiyo licha ya kwamba anataka kusalia. (Liverpool Echo)
No comments:
Post a Comment