Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro amethibitisha kufariki dunia kwa watu wanne akiwemo Ofisa Uvuvi wa Kanda ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza, Ibrahim Jalali baada ya kuzuka kwa vurugu baina ya wavuvi na Kikosi maalum cha kupambana na uvuvi haramu.
Akizungumza na EATV/EARadio Digital, Kamanda wa Muliro amesema hali ya vurugu ilitokea baada ya kikosi maalum cha watu watano kilichokuwa na Askari Polisi wawili wenye silaha za moto kugundua kuwepo kwa viasharia vya uvuvi haramu kwenye kisiwa cha Siza wenyeji ndipo walipovamiwa na Wanakijiji.
"Tuna kikosi kazi kinachofanya doria ya kudhibiti uvuvi haramu kwenye kisiwa cha Siza, kikosi kilifika pale baada ya kugundua kuna nyavu zinazotumika kwa uvuvi haramu, tukaamua kuzikamata na alipokuja Mwenyekiti wa Kitongoji kile akawaita wenye nyavu zao na walipo fika akawaamrisha kuanza kuwashambulia kikosi kile", amesema Kamanda Muliro.
Katika vurugu hizo, raia wanne akiwemo Ofisa huyo mvuvi wameuawa, ambapo raia hao wawili wamefariiki dunia baada ya kushambuliwa kwa risasi za moto na polisi waliokuwa kwenye doria hiyo.
Fuatilia mahojiano kamili hapo chini.
No comments:
Post a Comment