Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa, amethibitisha kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto Greyson Valentino, mwenye umri wa mwaka mmoja na kisha mwili wake kuutelekeza shambani.
Akizungumzia hali ya tukio hiyo Kamanda Mutafungwa amesema, tukio hilo lilitokea Julai 21 katika kijiji cha Hembeti Mvomero Mkoani humo, ambapo mwili wa mtoto huyo ulikutwa umefichwa kwenye shamba la mtuhumiwa huku ukiwa na majeraha kichwani.
Inaelezwa kuwa mara baada ya mtuhumiwa huyo mwenye miaka 8 kufikishwa Polisi, Jeshi hilo liliendelea na msako na kumkamata baba mzazi wa mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Said Stephen, aliyeunganishwa katika kesi inayomkabili binti yake ambapo imeelezwa kuwa baba huyo mara baada ya kupata taarifa za mauji aliyoyafanya mwanaye, alikimbia na hakutoa ushirikiano kwa polisi wala familia ya marehemu.
Kamanda Mutafungwa ameeleza namna ambavyo baba wa marehemu, alivyopokea taarifa za kupotea kwa mwanaye na katika harakati za kumtafuta walipita kwenye shamba la mtuhumiwa na kuukuta mwili wa mtoto wake ukiwa na majeraha kichwani.
Inaelezwa kuwa walipofika nyumbani kwa mtuhumiwa kwa nia ya kuhoji sababu ya mwili wa mwanaye kukutwa kwenye shamba lake, ndipo mdogo wa mtuhumiwa alipobainishwa namna alivyoshuhudiwa dada yake, akimuua baada ya kumpiga na panga kichwani kisha kumuweka shambani.
Kufuatia hali hiyo mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa polisi na baada ya kuhojiwa alikiri kufanya tukio hilo.
No comments:
Post a Comment