Mchezo wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Platinum Stars uliopigwa leo huko Afrika Kusini, umemalizika kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara kuibuka na ushindi wa mabao 4-1
Mabao mawili yaliyofungwa na Clatous Chama, bao la mkwaju wa penati lililowekwa kambani na Sharaff Shiboub na bao la Mzamiru Yassin yalitosha kuipa Simba ushindi wa pili wa mabao manne
Katika mchezo huo, kocha Patrick Aussems aliwapa nafasi wachezaji wote
Mbelgiji huyo amesisitiza kuwa anatumia michezo hii ya kirafiki kuunda kikosi cha kwanza
Simba itacheza michezo mingine miwili dhidi ya Township Rollers (July 27) na Orlando Pirates (July 30) kabla ya kurejea nchini tayari kwa Simba Day August 06
No comments:
Post a Comment