Taarifa za awali zinaeleza kuwa wachimbaji hao wamefukiwa na kifusi cha mchanga wakati wakichimba madini aina ya dhahabu ambayo yameibuka siku za hivi karibuni katika Kijiji cha Iyogwe wilayani Gairo.
Akizungumza leo Jumapili Juni 9, 2019, Mwenyekiti wa chama cha wachimba madini Mkoa wa Morogoro, Dk Omary Mzeru amesema wamepata taarifa hizo na sasa wanafuatilia zaidi.
Mwananchi lilipomtafuta Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe amesema yeye na kamati yake ya ulinzi na usalama wanaelekea eneo la tukio.
Taarifa zaidi kuhusu tukio hili endelea kufuatilia hapa hapa
No comments:
Post a Comment