We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 7, 2019

Usajili Yanga wamuibua Makamba


KWA sasa habari ya mjini ni namna Yanga inavyoendelea na fujo zao za kushusha nyota mbalimbali kwa ajili ya usajili wa msimu ujao, sasa kumbe usajili huo unafuatiliwa na shabiki wa kutupwa wa Simba, Yusuf Makamba ambaye ameamua kuvunja ukimya.

Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji saba ambao ni Lamine Moro, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Kalengo Maybin, Mustapha Seleman, Abdul Azizi Makame.
Mzee Makamba aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amesema ni kweli Yanga wanatamba kwenye usajili, lakini  amewataka mashabiki wenzake wa Mnyama wasiwe na wasiwasi na usajili wa mbwebwe 3unoafanywa na watani wao Yanga kwa sababu ni wa kawaida tu.
Alitoa maoni yake hayo jana Ijumaa alipozungumza na Mwanaspoti kijijini kwake Mahezangulu wilayani Lushoto.
Katibu huyo Mkuu Mstaafu wa CCM ambaye ni humwambii kitu kwa Simba ambao ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu pamoja na Coastal Union ambayo pia huishabikia kama timu yake ya nyumbani.
Makamba alisema hatishwi kabisa na  usajili huo wa watani wao kwa sababu timu yao imekamilika na kama hata wasiposajili  hakuna timu ambayo itawazuia kuwa mabingwa hapa nchini.
Alisema Simba ina wachezaji wazuri wengi tofauti na watani wao kitu cha muhimu wanachotakiwa kukifanya ni kufundishwa vizuri  na kuandaliwa kwa uhakika jambo ambalo litawapelekea kutwaa tena ubingwa wa ligi na wa Afrika ambapo Simba imepata nafasi tena ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
“Ukitaka kujua kuwa  Simba ina wachezaji wengi hata kama isipo sajili itafanya vizuri wewe angalia mechi  kati yake na ile timu ya kutoka Hispania ya Sevilla ambayo tulipoteza kwa mabao  5 – 4 lakini walikiona cha mtema kuni," anasema Makamba
Mwanachama huyo alisema hana wasiwasi  na Simba kwani ina viongozi wazuri hivyo watafanya usajili wa maana tofauti na watani zao.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list