Mshambuliaji wa Simba Adam Salamba amesema anahitaji kupata nafasi ya kucheza ili kulinda kipaji chake hivyo atakuwa tayari kwenda kucheza timu yoyote kama mabosi wa Simba wataamua kumtoa kwa mkopo
Salamba aliyetua Simba kutoka Lipuli Fc, amekuwa na msimu mgumu akishindwa kupata nafasi mbele ya washambuliaji vinara wa mabao Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi
Kumekuwa na tetesi kuwa mshambuliaji huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo
"Mimi ni bado ni mchezaji wa Simba, nina mkataba hivyo siwezi kuindoka bila uamuzi wa viongozi wangu," amesema Salamba
"Kikubwa nawasikiliza mabosi kama watanitoa kwa mkopo sawa tu na kama nikibaki nitahakikisha napambana ili nitate nafasi ya kucheza msimu ujao"
Simba inatarajiwa kukiboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao
No comments:
Post a Comment