Kiungo fundi wa Simba Jonas Mkude amesema hafikirii kuondoka kunako klabu hiyo kwani anaamini bado wakati wa kufanya hivyo haujafika
Mkude alikuwa akihusishwa kusajiliwa na Yanga kabla ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' kumaliza tetesi hizo kwa kuwahakikishia Wanamsimbazi kuwa mwamba huyo haendi kokote
Mkude ni miongoni mwa wachezaji waliomaliza mikataba ambapo michakato ya kuhuisha mikataba yao inaendelea
Licha ya kuendelea kuhusishwa na Yanga, Mkude amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote kwa kuwa hajafanya mazungumzo na kiongozi yeyote wa timu hiyo
"Sijafanya mazungumzo na timu yoyote zaidi ya Simba. Kuhusu kuondoka Simba sifikirii kwani naamini bado mchango wangu unahitajika lakini wakati wa kuondoka ukifika nitaondoka," amesema
Juzi Mkude alienguliwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichokwenda Misri kushiriki michuano ya AFCON
Uamuzi wa kocha Emmanuel Amunike kumuengua Mkude pamoja na Ibrahim Ajib umewakera wadau wa soka nchini kwani kwa uwezo walionao wachezaji hao, walipaswa kuwemo katika kikosi kitakachoshiriki AFCON
No comments:
Post a Comment