Rais wa Tanzania, John Magufuli amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwakamata watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuwapeleka mahakamani.
Watumishi hao wanatuhumiwa kukamata mizigo ya mfanyabiashara tangu mwaka 2017 bila sababu wakitaka rushwa.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo June 7, 2019 wakati alipokutana na wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini Ikulu jijini Dar es Salaam na kuzungumza nao ambapo wamemueleza changamoto zao.
Kuhusu sakata hilo Rais Magufuli amemtaka Kamshna wa TRA kuwasimamisha kazi watumishi hao. Sambamba na hilo, Rais ameagiza TRA kumlipa fidia mfanyabiashara huyo ambaye mzigo wake ulishikiliwa kwa miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment