Mechi mbili za mtoano 'Plyaoff' zilizokuwa zichezwe leo hii kati ya Pamba FC dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold dhidi ya Mwadui zimeahirishwa na badala yake zitachezwa kesho majira ya saa kumi jioni.
Taarifa zinaeleza kuwa mchezo huo umeahirishwa wakati timu zikiwa uwanjani muda mfupi kabla ya mchezo kuanza.
Mmoja wa viongozi wa Pamba FC, Mohamed Mutabora ambaye ni (Msemaji Msaidizi wa Pamba) amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo yalikuwa yameshakamilika kuanzia kwenye 'pre-match meeting' hadi kwenye kupasha misuli kabla ya mchezo, lakini wameshangazwa baada ya kupigiwa simu na uongozi wa uongozi wa Bodi ya Ligi wakiambiwa kuwa mchezo umeahirishwa.
"Wanatuambia sababu ni kuwa tumegoma mechi isioneshwe lakini sio kweli lakini wanasema nyie mmekubali lakini Geita Gold wamegoma wakati sisi na wao hatuko kundi moja", amesema.
Msimamizi wa kituo ambaye pia ni Katibu wa chama cha soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo amesema kuwa ni kweli mchezo umeahirishwa na utarudiwa kesho lakini sababu itatolewa na uongozi wa Bodi ya Ligi.
Tazama msemaji msaidizi wa Pamba FC akizungumza.
No comments:
Post a Comment