Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo, amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kalambo kuwasaka na kuwatia nguvuni wananchi wanaosadikiwa kuhujumu miundombinu ya maji katika Kijiji cha Kisongamile, ambacho kipo jirani na ujenzi unaoendelea wa Hospitali ya Wilaya ya Kalambo, hali inayopelekea
kurudisha nyuma kasi ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema kuwa Hospitali hiyo ni ya kwao na kwamba wao ndiyo wa kwanza kufaidika nayo pindi itakapokamilika, hivyo amemtaka Mkuu wa Wilaya kuhakikisha analimaliza tatizo hilo ndani ya muda mfupi ili kuendana na ratiba ya umaliziaji wa ujenzi wa Hospitali hiyo.
"Nimeona hii changamoto ya maji pamoja na kwamba wanachimba kisima, lakini kile kijiji pale ambacho kinakwamisha kinahujumu miundombinu ya maji Mhe. DC pamoja na kamati ya usalama muende pale, pamoja na mwenyekiti wa halmashauri, mkazungumze na kile Kijiji." amesema Wangabo
"Lakini pia kama kuna watu ambao wanadhaniwa wanahujumu kwa makusudi miundombinu, haiwezekani Kijiji kizima kikawa kinahujumu miundombinu, mchukue hatua ya kuwakamata hao wote wanaohujumu miundombinu ya maji." amesisitiza Mkuu huyo Mkoa Wangabo. amesema Wangabo
No comments:
Post a Comment