We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, June 8, 2019

Mbunge wa zamani wa jimbo la Lindi atimkia CHADEMA


Na Ahmad Mmow, Lindi.

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Lindi kwa tiketi ya CUF, Salum Barwany leo amehama chama hicho na  amejiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).

Habari kutoka ndani ya ukumbi wa mikutano wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) uliopo katika manispaa ya Lindi ambamo amekabidhiwa kadi ya CHADEMA.Huku ikielezwa kuwa Barwany amekabidhiwa kadi hiyo na mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Imebainshwa kwamba Barwany ambae pia alikuwa mwenyekiti wa CUF wa wilaya ya Lindi  alikabidhiwa kadi hiyo na mwenyekiti Mbowe wakati wa kikao cha ndani. Ambacho pia kimehudhuriwa na naibu katibu mkuu wa Chama hicho,  Salum Mwalimu.

 '' Nikweli mheshimiwa Barwany tulikuwa nae tangu asubuhi humu ukumbini, muda si mrefu amekabidhiwa kadi na mwenyekiti, mheshimiwa Barwany ameshatoa neno,'' kimedokeza chanzo makini kilichopo ndani ya ukumbi huo.

Bado haijafahamika washiriki wa kikao hicho ni akina nani na kilikuwa kinahusu nini, Kwani hakuna mwandishi wa habari aliyealikwa au kuruhusiwa kuingia kwenye kikao hicho cha ndani.

Aidha juhudi za kumpata mheshimiwa Salum Barwany na viongozi wa chama hicho ili wathibitishe hazikufanikiwa. Kwani bado walikuwa ukimbini wakiendelea na kikao.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list