"Mimi kama nimejenga majengo basi na wao wahangaike kuleta madawati lakini wakisubiri uchaguzi (wa 2020) mimi nikiwepo wahesabu maumivu,” amesema Makonda.
Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Juni 8, 2019 katika uzinduzi wa ofisi za walimu Shule ya Msingi Vijibweni Wilaya ya Kigamboni zilizojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya CRJE (East Africa) Limited ya China.
"Wako wabunge wanaojiona wa kimataifa hawahangaiki na kero za wananchi wala hawataki kufanya ziara wanasubiri wakapige kelele bungeni na kujirekodi," amesema Makonda.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema wabunge hao wamezoea ukibaki mwaka mmoja kuelekea uchaguzi mkuu ndio huanza kujipitisha na kusikiliza kero za wananchi, akibainisha kuwa safari hii wahesabu maumivu.
Meneja ujenzi tawi kampuni hiyo, Bai Hao Chein amesema wameamua kujenga ofisi hiyo ili kupanua kiwango cha elimu.
Amesema wamekuwa wakitoa misaada kwa lengo la kudumisha urafiki kati ya serikali ya Tanzania na China.
"Tutaendelea kutoa misaada kutokana na kampuni kushiriki katika miradi mikubwa na Serikali ya Tanzania ikiwemo ujenzi wa Jengo la Bunge pamoja na daraja la Mwalimu Nyerere," amesema Chein.
Jengo hilo lenye uwezo wa kukaa walimu 60 pamoja na ofisi ya mwalimu mkuu limegharimu zaidi ya shiilingi 200 milioni.
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Mkoa wa Dar es Salaam, ACP Solomon Urio amesema majengo 28 kati ya 402 yamejengwa na ofisi 18 ziko katika hatua mbalimbali.
"Zipo ofisi na majengo yameshakamilika katika Wilaya nyingine, majengo mengine 18 yapo katika hatua mbalimbali kukamilika,” amesema Urio.
No comments:
Post a Comment