Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, bado hajalisahau tukio la kutekwa kwake lililozua sintofahamu mwaka jana
Tarehe 11 Oktoba 2018 itabaki katika kumbukumbu ya Watanzania wengi kwani alfajiri ya siku hiyo ndio taarifa za kutekwa Mo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii
Mo alitekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar es salaam
Hata hivyo tukio hilo limemuimarisha zaidi Mo, mwenyewe amesema limemsogeza karibu zaidi na Mungu
"Unapopitia kipindi kigumu, unajuaje kama Mungu anakujaribu au anakuhukumu?," ameandika Mo kwenye ukurasa wa mtandao wa Instagram
"Jibu ni linalokusogeza karibu na Mungu ni jaribu. Ambalo linakupeleka mbali na Mungu ni adhabu. Ukweli ni kwamba, kutekwa kumenisogeza karibu sana na Mungu"
Mpaka sasa mshukiwa mmoja ameshafikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya kumteka Mo
Mwishoni mwa mwezi Mei, dereva teksi Mousa Twaleb alifikishwa mahakamani akihusishwa na tukio hilo
Twaleb alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Jumanne ya Mei 28, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kumteka Mo
No comments:
Post a Comment