Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Dk. Chrisant Mzindakaya amesema Wizara ya Kilimo nchini Tanzania inaliangusha Taifa hilo tangu lilipopata uhuru wake mwaka 1961.
Dk Mzindakaya amesema kilimo ni sayansi na sio hotuba, na kwamba ni ngumu kusema mahindi oyee na yakawa oyee kweli.
“Kilimo ni sayansi tena kitaalamu taasisi zote za kilimo katika wizara hii zinakufa na ushahidi ni Uyole-Mbeya ilikuwa inawika leo ni taabani sasa kilimo kitaendeleaje, ” amesema Kada huyo wa CCM leo, wakati akizungumza katika mkutano kati ya Rais Magufuli na wafanyabiashara kutoka Wilaya zote nchini uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
“Huyu Waziri mpya (wa Kilimo) aamke, nilishamueleza nipo tayari kumshauri na hao vijana wako wakubali wazee tuwape ushauri naweza kusaidia bado, wala siombi kazi kwa mtu mimi nitasaidia maana ninapenda unavyoendesha nchi.” amesema Dk Mzindakaya.
Aidha Mzee huyo amemshauri Rais John Magufuli kutoa nafasi kwa kila waziri kuchagua jambo moja atakaloliletea sifa Tanzania kwa sababu hawawezi kufanya kila kitu.
Mzee huyo amekuwa katika Bunge kwa miaka 44.
No comments:
Post a Comment