Kagera Sugar na Mwadui Fc zimefanikiwa kutetea nafasi zao za kubaki ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kushinda michezo yao ya Playoff
Mwadui Fc imefanikiwa kuwalaza majirani zao Geita Gold kwa mabao 2-1, Salum Aiyee akiibuka nyota wa mchezo huo baada ya kuifungia timu yake mabao yote mawili
Bao la ushindi alilifunga kwenye dakika ya 90 na kuinusuru Mwadui Fc na hatari ya kuteremka daraja kwani kama mchezo huo ungemalizika kwa sare ya bao 1-1 Mwadui ingeshuka
Nayo Kagera Sugar imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba katika mchezo uliopigwa uwanja wa Kaitaba
Mabao ya Ali Ramadhani na Japhet Makalai, yaliihakikishia Kagera Sugar kubaki ligi kuu
Pamba na Geita Gold zimehitimisha harakati za kuwania nafasi ya kupanda ligi kuu bila ya mafanikio
Namungo Fc na Polisi Tanzania ndio timu pekee zilizopanda ligi kuu kutoka ligi daraja la kwanza wakati Stand United na African Lyon zimeshuka ligi daraja la kwanza
No comments:
Post a Comment