We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, June 8, 2019

BREAKING: Rais Magufuli Amtumbua Waziri wa Viwanda na Biashara na Kamishna Mkuu wa TRA.


 Rais wa Tanzania, John Magufuli amemteua Innocent Bashungwa, kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, akichukua nafasi ya Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi JUni 8, 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa amesema Rais Magufuli amemteua Edwin Mhede kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akichukua nafasi ya Charles Kichere.

Msigwa amesema Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe akichukua nafasi ya Erick Shitindi ambaye amestaafu.

Aidha kabla uteuzi waziri mpya wa viwanda na Biashara Innocent Bashungwa alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Kamishna Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Edwin Mhede kabla ya uteuzi huu, alikuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
Ikulu imeeleza uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara utafanywa baadae.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list