Ajib ni miongoni mwa nyota saba walioenguliwa katika msafara wa kwenda Misri kwenye mashindano ya Fainali za Afcon, wengine ni Ayub Lyanga, Ally Ally, Kennedy Wilson, Kassim Khamis, Jonas Mkude na Shomari Kapombe.
Ngassa alisema amelipokea kama changamoto suala la kutolewa katika kikosi cha timu ya taifa na kuweka wazi anaimani na nyota waliobaki anaamini wanaweza kufanya vyema katika mashindano hayo.
Pia, aliongeza kwa kuwaomba Watanzania kuwa na imani na nyota waliobaki kwani wameonyesha kitu tofauti na wao na ndio maana wameweza kubaki kwa lengo la kuiwakilisha nchi hivyo kwa upande wake ataendelea kuwaunga mkono akiwa nje ya kambi kama kunakitu kitahitajika kutoka kwa nyota wenzake.
Alipoulizwa kuhusiana na suala la kutega mazoezini Ajib alisema alifuata program yote ya mwalimu kuanzia mwanzo wa mazoezi hadi siku anaondolewa kikosini hivyo sababu hiyo haiwezi ikawa inamuhusu yeye.
"Nimeingia kambini kama ilivyopangwa na nimehuzuria mazoezi yote kama ilivyokuwa inatakiwa sijajua niwapi nimekosea hadi nimeondolewa huenda siona sifa za uchezaji anazozitaka mwalimu nimelipokea kama changamoto nitaendelea kupambana kwa lengo la kusaka tena namba ya kucheza Taifa Stars," alisema Ajib.
No comments:
Post a Comment