Wanasheria na Mawakili wa chama hicho leo Aprili 06, 2019 wanapiga kura kumchagua Rais Mpya wa chama atakayechukua nafasi ya Mwanasheria Fatma Karume anayeelekea kumaliza muda wake.
Wagombea wa Urais waliopitishwa na Kamati ya uteuzi Machi 5, ni John Seka aliyeongoza chama hicho 2016/17 na Makamu wa Rais wa chama hicho, Dkt. Rugemeleza Nshala.
Wengine ni Godwin Ngwilimi aliyekuwa makamu wa Rais katika uongozi wa Tundu Lissu na Godfrey Wasonga aliyejitokeza kwa mara ya pili mfululizo kugombea nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment