USAJILI : Simba hawashindwi wanasa moja ya beki bora Afrika
Kuendelea kufanya vibaya kwa wapinzani wao katika ligi wapinzani ambao walianza ligi kiasi cha kuwatisha kunazidi kuwapa matumaini Simba ya kutwaa tena Ubingwa wa ligi kuu msimu huu hivyo kuwa na nafasi ya kushriki kimataifa kwa mara nyingine.
Simba ikishinda mechi zake zote za ligi na Yanga ikishinda mechi zake zote za ligi kuu basi Simba ndiye atakayekuwa Bingwa tena kwa tofauti ya alama takribani 10.
Sasa usajili wa Simba kwaajili ya msimu ujao mipango yao unaambiwa si ya kitoto kabisa kwani wanataka wasajili wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuwasaidia katika michuano ya kimataifa ambao kikawaida kwenye ligi itakuwa Laini tu.
Yule beki katili anayecheza kwa nguvu na akili nyingi wa As Vita Yannick Bangala Litombo inaelezwa kuwa yupo katika rada za Simba na huenda msimu ujao akavaa jezi nyekundu na nyeupe za wana Msimbazi Simba.
Mchezaji huyo ni beki wa kati mwenye umri wa miaka 24 lakini April 14 atakuwa anafikisha miaka 25 anaurefu wa mita 1.88 uraia wake ukiwa ni wa Congo.
Mchezaji huyo amewahi kucheza Les Stars ya Congo, Dc Motema Pembe na kisha akajiunga na As Vita ambayo amecheza nayo kwa mafanikio na kutajwa mara kadhaa kama moja ya mabeki bora wa kati barani Afrika kwasasa.
No comments:
Post a Comment