We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, April 1, 2019

TP Mazembe kwisha, 'wadukuzi' wapewa kazi maalum

Baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbao FC mjini Morogoro, kocha wa klabu hiyo, Patrick Aussems ametuma salamu kwa TP Mazembe kuwa tayari benchi lake la ufundi linafuatilia kwa karibu video zao.


Kocha wa Simba, Patrick Aussems
Kocha Aussems amesema kuwa kabla ya kuwavaa Mazembe, kuna mchezo mmoja Jumatano ya wiki hii dhidi ya JKT Tanzania ambao atafanya mabadiliko ya kikosi ili kila mchezaji awe sehemu ya mchezo.
"Ni siku mbili zimebakia kabla ya mchezo na TP Mazembe maana tunacheza nao Jumamosi na ukitizama ni siku chache mno zilizobakia lakini viongozi wenzangu wa benchi la ufundi wanatizama video za wapinzani wetu", amesema Aussems.
Simba itacheza na JKT Tanzania Jumatano kabla ya kurejea Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Congo DR Jumamosi, April 6 katika Uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Mchezo wa hapo jana, Simba imefikisha jumla ya mechi 10 mfulululizo za ushindi katika Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo. Kupitia ukurasa wa Twitter, kocha Patrick Aussems amewapongeza wachezaji na msahabiki kwa kuifikia rekodi hiyo.



View image on TwitterView image on TwitterView image on Twitter

Good job guys ! 10th victory in a row in TPL , that's the 1st time in Simba's history ... let's go and take an 11th one on wednesday against JKT . Thanks to all our Morogoro's fans !!

138 people are talking about this

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list