Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba, 26, ambaye bado anahusishwa na Real Madrid anataka mshahara wa pauni 500,000 ili kuendelea kubaki Old Trafford. (Sun). Winga wa Bournemouth na Scotland Ryan Fraser, 25, amesema amefurahishwa kuhusishwa na usajili kuelekea Arsenal. (Sky Sports)
Klabu ya Queens Park Rangers sasa wanamnyemelea kocha wa zamani wa Tottenham na Aston Villa Tim Sherwood kuwa mrithi nambari moja wa kocha Steve McClaren. (Standard)
Paris St-Germain wapo tayari kumlipa kipa David de Gea, 28, mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki. Kipa huyo wa Manchester United bado hajasaini mkataba mpya na klabu yake na inaaminika kuwa kiwango cha mshahara ndicho kinacho chelewesha kusainiwa kwa makubaliano mapaya. (Independent)
Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anapendelea kusajili wachezaji wengi zaidi kutoka Uingereza. Na mpaka sasa anawanyemelea kiungo wa West Ham Declan Rice, 20, winga kinda wa Chelsea Callum Hudson-Odoi 18, pamoja winga wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21. (Times)
Fulham watakubaliana na hali ya kumpoteza mchezaji wao kinda Ryan Sessegnon, 18, ambaye anauwezo wa kucheza kama beki ama winga wa kushoto. Fulham tayari wameshashuka daraja kenye ligi ya Primia. (Standard)
Klabu hiyo pia italazimika kumrudisha kwa mkopo mshambuliaji wao raia wa Ujerumani Andre Schurrle katika klabu ya Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu. (Sun)
Real Madrid wamo katika mbio za kumsajili beki wa kati wa Manchester United na Ivory Coast Eric Bailly, 24, kwa kitita cha pauni milioni 35. (Sun)
Mshambuliaji Jermain Defoe, 36, amesema kuwa ataendelea kusalia kwa mkopo katika klabu ya Rangers ya Uskochi msimu ujao badala ya kurudi kwenye klabu yake mama ya Bournemouth. (Daily Record)
Kocha wa Newcastle Rafael Benitez ameiajiri mapuni moja ili imsaidie kupata kazi kwenye klabu za juu nchini Ufaransa. (L’Equipe, via Chronicle)
Mshambuliaji kinda wa Birmingham na Uingereza Romello Mitchell, 16, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Southampton. (Birmingham Mail)
No comments:
Post a Comment