Sakata kuhusu mchanga wa makinikia, ubaguzi wa kiitikadi na kufungwa kwa maduka ya fedha jana yaliibuka bungeni wakati wa mjadala hotuba ya bajeti ya Ofisi ya waziri Mkuu, wakati wabunge walipotaka masuala hayo yaangaliwe upya.
Jana, mbunge wa kuteuliwa na Rais, Abdallah Bulembo aliishauri Serikali kuruhusu watu kusafirisha mchanga huo badala ya kuendelea kuwazuia.
Bulembo alisema kuwazuia kusafirisha nje kunasababisha Serikali ikose mapato na pia kuathiri wachimbaji ambao hawana madoa.
Wakati Bulembo akiibuka na makinikia, mbunge wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Jaku Hashim Ayub aliitaka Serikali kuweka masharti yenye uwiano katika biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni.
No comments:
Post a Comment