Jumapili Rwanda itaanza kumbukumbu za miaka 25 za mauaji ya kimbari. Watu 800,000 wengi wao Watutsi walipigwa, na wengine kuuawa katika kipindi cha siku mia moja. Robo karne baadaye nayaliyotokea hayajasahaulika.
Kama ilivyozoeleka, kila Aprili 17 ambayo itakuwa Jumapili kwa mwaka huu - siku mauaji hayo ya kimbari yalipoanza- Rais Paul Kagame atawasha mwenge wa kumbukumbu katika Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari kwenye mji mkuu wa Kigali ambako inaaminika zaidi ya waathirika 250,000 walizikwa hapo.
Siku hiyo itakuwa ndiyo mwanzo wa kumbukumbu hizo ambazo zitakuwa na matukio kadhaa yatakayodumu kwa siku mia moja zijazo zilizotengwa kusudi kwa maombolezo ya nchi nzima.
Mchana wa siku hiyo hiyo ya Jumapili, Kagame ambaye aliwaongoza waasi waliopambana na wanamgambo na wanajeshi wa serikali na kubaki madarakani kama kiongozi wa taifa tangu wakati huo, ataongoza hafla ya kumbukumbu katika kiwanja cha soka mjini Kigali.
Ingawa miaka 25 imeshapita, lakini yaliyotokea yameacha mabaki yake. Jean-Paul Haguma, ni mwanafunzi wa miaka 26, na anasema mabaki ya mauaji hayo bado yangaliko na kuonekana dhahir katika jamii za nchini humo.
"Tunaishi na matokeo ya mauaji ya kimbari ambapo unakuta baadhi ya watu wametengwa na familia zao au labda hata hawana familia. Wahalifu, waathirika na hata wale ambao hawakuwa wamezaliwa wakati huo, basi wote wanakabiliwa na matokeo sawa," amesema Haguma.
No comments:
Post a Comment