Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Viwanda, Stella Manyanya wajitathmini katika utendaji wao wa kazi.
Katika hotuba yake jana, Rais alimtaka Profesa Mbarawa akae na wataalamu wake kwa sababu wamekuwa wakifanya vibaya na miradi mingi ya maji haikamiliki .
“Nilikupeleka Wizara ya Maji ukafanye mabadiliko, lakini bado unashindwa kuwachukulia hatua wahandisi wa maji ambao hawasimamii kikamilifu miradi ya maji,” alisema Rais Magufuli jana wakati akizungumza na wananchi wa Tunduru mkoani Ruvuma katika ziara yake ya kikazi.
“Haifurahishi kuona wananchi wanalalamikia ukosefu wa maji, ni uzembe. Wafukuze wakandarasi wa maji na chukua hatua kwa mainjinia wa maji ambao wanafanya vibaya, ukiwa mpole miradi haitakamilika.” Alisema Rais Magufuliania na Msumbiji ambao ni Mto Ruvuma usiokauka.”
Rais Magufuli pia alionesha kukerwa na Naibu Waziri Manyanya kwa kushindwa kufuatilia kiwanda cha kubangua korosho kilichopo Tunduru ambacho kilikuwa na uwezo wa kubangua tani 5,000 hadi 15,000 lakini mwaka jana kilibangua tani 3,500.
“Naibu Waziri wa Viwanda upo hapa na hili limekushinda kufuatilia, na hapa ni nyumbani kwako umeshindwa kusimamia hiki (kiwanda) kilichokuwa cha Serikali na kimebinafsishwa kwa kwa bei ya kutupwa milioni 75 wakati ni cha mabilioni, utaweza kusimamia viwanda vya Dar es Salaam? Unasubiri mimi ndio nifuatilie?” alihoji.
No comments:
Post a Comment