Aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva kutoka THT, Jessie, amefariki dunia. Jessie ni dada wa msanii, Jolie. www.eatv.tv imemtafuta mmoja kati ya wasanii kutoka THT, Mwasiti Almas ambaye amesema ni kweli kuwa msanii huyo amefariki dunia.
Jessie enzi za uhai wake.
Hata hivyo Mwasiti hakuelezea chanzo cha kifo chake kutokana na kutokuwa sehemu rafiki kwaajili ya mazungumzo na kuahidi kuwa ataeleza taarifa zaidi.
"Ni kweli Jessie amefariki, lakini sipo sehemu nzuri kuzungumza kuna kelele sana", amesema Mwasiti.
Marehemu Jessie enzi za uhai wake amewahi kufanya kazi kadhaa ikiwemo nyimbo ya 'Mapenzi Kamali' aliyomshirikisha Madee. Kwa mujibu wa taarifa za awali, kifo chake kimetokea hospitali wakati wa kujifungua
No comments:
Post a Comment