Rais mpya wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika Dkt Rugemeleza Nshala amesema katika uongozi wake atahakikisha Mawakili atakaowaongoza anawapatia mafunzo na kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya kazi.
Fatma Karume
Dkt Nshala ametoa kauli hiyo Arusha mara baada ya kushinda nafasi ya Urais wa chama hicho akipokea kijiti kutoka kwa Fatma Karume, ambaye amemaliza muda wake baada ya kukiongoza chama hicho kwa mwaka mmoja.
"Tutapigania sheria kwa nchi yetu, na tutawaendeleza wanachama wetu waweze kufanya kazi kwa uhuru bila kunyanyaswa kutishwa na kuwekwa ndani kama ilivyojitokeza hivi sasa, Mawakili ni watu muhimu kuhakikisha nchi yetu inatawaliwa kisheria" amesema Dkt Nshala
Dkt Rugemeleza Nshala ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 629 kati ya wajumbe 1162 ambapo pia miongoni mwa miongoni mwa wajumbe ambao walichaguliwa kwenye nafasi ya Wajumbe wa Baraza la chama hicho ni Wakili Jebra Kambole.
Uchaguzi wa TLS umefanyika April 7, 2019 ambapo Rais aliyemaliza muda wake ni Fatma Karume ambaye alipokea kijiti kutoka kwa Mbunge Singida Mashariki Tundu Lissu.
No comments:
Post a Comment