Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kwake yeye haoni tija ya kuendelea kuongeza idadai ya Mikoa nchini ili kutoa nafasi kwa serikali kuweza kufikisha maendeleo kiurahisi kwa wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa wilayani Tunduru mkoani wa Ruvuma alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara ya Tunduru - Namtumbo ambapo amesema katika kipindi cha utawala wake, hataongeza Mkoa.
"Hata kuwepo kwa mikoa yote hii ishirini na kitu kwa mawazo yangu mafupi hapakuwa na sababu, tungeweza kuwa na mikoa michache, zile gharama za kuendeshea mikoa tungezipeleka kwa maslahi ya wananchi, tukajenga hospitali na tukapeleka madawa na wakawa na magari ya wagonjwa." amesema Rais Magufuli.
Aidha kuhusiana na ujangili wa tembo, Rais Magufuli amesema kuwa, "washtakiwa wengi wanaua tembo wetu, wakiua tembo kule wanawaleta huku wakiua huku wanawapeleka kule mtandao wote tushaujua mkae mwendo wa mchakamchaka, wako wengine wanashirikiana na viongozi."
Rais Dkt John Pombe Magufuli leo Aprili 5, 2019, anaanza ziara ya kikazi ya siku 6 Mkoa wa Ruvuma akitokea mkoani Mtwara ambapo alifanya ziara ya siku 3.
No comments:
Post a Comment