Joto la mchezo wa klabu bingwa kati ya TB Mazembe ya Congo na Simba ya Tanzania limeandelea kuongezeka kila kona. Mchezo huo unachezeka leo majira ya saa 10 jioni katika uwanja wa Taifa.
DC wa Kisarawe, Jokate Mwegelo ambaye ni shabiki kindaki ndaki, Yanga SC amewauliza mashabiki wenzake wa Jangwani kwamba ataruhusiwa leo kuvaa jezi ya Simba ili achukue tsh milioni 20 aliyoahidiwa na msemaji wa Simba Haji Manara.
“Kwenye Harambee yetu ya #TokomezaZeroKisarawe Gala Jumamosi iliyopita Msemaji maarufu sana Afrika wa klabu ya Simba @hajismanara aliahidi yeye pamoja na rafiki zako watatoa Shillingi Milioni 10.
Lakini pia akasema iwapo leo nitakaa nae kwenye mechi ya Simba dhidi ya TP Mazembe nikavaa jezi ya Simba atatoa Milioni 10 nyingine kwa ajili ya ujenzi. Kumbuka mimi ni Yanga.
Wanazengo naombeni ushauri nivae jezi ya Simba leo nikachukue Milioni 20 kwa ajili ya wananchi wa Kisarawe? Kumbuka pia mimi ni kiongozi wa wananchi wote wanaoshabikia timu mbalimbali lazima niwatendee haki. Naomba ushauri jamani 😄”

Baada ya kuandika ujumbe huyo kupitia Instagram yake, mashabiki wake amemshauri ahamie kabisa msimbazi. Angalia maoni ya mashabiki.
soggydoggyanter
Hamia kabisa sio kuvaa jezi tu 😂😂😂 @jokatemwegelo
mdoe_irene
Anything for tokomeza zero..anything for our pretty girls….. millioni 10 …ni mashimo ya vyoo kma yootee 😂 ….. plz a tshirt for few hours wont hurt kiongozi.
so_nakshii
vaa DC uzalendo kwanza sisi ni watani sio maadui🙌🙌🙌🙌🙌
mbomaveronica
Tatizo manara simuamini unawez kuvaa na hela asitoe yule hahahha
No comments:
Post a Comment