We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, April 5, 2019

Harry Kane kuwatoa wachezaji wa England Uwanjani kama watabaguliwa


Ukiachilia mbali nyota wa Juventus Moise Kean kubaguliwa huko Italia hivi karibuni wachezaji wa timu ya taifa ya England wenye ngozi nyeusi walibaguliwa kwa kupigiwa kelele za nyani wakati wakicheza mchezo wa kuwania kucheza fainali za Euro 2020 dhidi ya Montenegro ugenini. 

Baadhi ya wachezaji hao waliobaguliwa ni pamoja na Danny Rose na Raheem Sterling, nahodha wao Harry Kane ametangaza rasmi msimamo wake kuhusiana na wachezaji wake wa timu ya taifa ikitokea wakaoneshwa au kufanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi basi atatoa timu yote nje ya uwanja. 

“Nitaitoa timu yote ya England Uwanjani kama wachezaji watakutana na changamoto za kuendelea kufanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi, sasa ni juu yao kwa wahusika kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa kwa wale watu watakaofanya vitendo hivi kwa sababu havikubaliki katika soka au sio sehemu ya maisha” alisema Harry Kane 

Kane ameeleza hisia zake kuwa haoni tatizo kukemea hali hiyo kwa kutoka nje ya uwanja kwani sio kitu kizuri, wengi wamempongeza Harry Kane kwa kuonesha ujasiri wa kutetea haki za wachezaji wenzake ambao wana asili ya ngozi nyeusi japokuwa yeye hayupo katika kundi la wachezaji ambao wanaweza kukutana na changamoto. 

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list