Msemaji wa Simba SC, Haji Manara amemkingia kifua nahodha wa timu hiyo, John Bocco baada ya kukosa mkwaju wa penalti hapo jana kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe.
Haji amesema kitendo cha Bocco kushindwa kufunga penalti hiyo ni sehemu tu ya mchezo na hakuna haja ya kumlaumu ikiwa wachezaji wakubwa nao hushindwa. Chini ni kile alichoandika Haji Manara;.
Ni mpuuzi tu atakayemlaumu John Bocco kukosa Penati, ni ugeni katika mpira kwa baadhi yetu. Boko huyu huyu ndio anafunga Penati zote za Simba kila tunapopata!! Boko huyu huyu ndio alifunga Penati muhimu kule kitwe tulipocheza na Nkana!!.
Penati ni pigo la bahati na huwa haina mwenyewe, ikiwa Messi mwenye mpira wake hukosa, Captain John Bocco ni nani asikose? Halaf ikumbukwe huyu kakosa na Mazembe, kuna mtu juzi tu kakosa na Ndanda!!.
Tuwape nguvu wachezaji wetu ili wakapambane kule Lubumbashi,tuache lawama za hovyo hovyo - Haji Manara Msemaji wa Simba SC. Mwisho wa kunukuu.
Kwa matokeo ya jana ya kustoshana sare ya bila kufungana dhidi ya TP Mazembe, Simba SC wanahitaji ushindi au sare yoyote ya magoli ili kutinga hatua ya nusu fainali ya klabu Bingwa Afrika.
No comments:
Post a Comment