Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga leo wameingia kambini Hotel ya Nefaland kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kombe la FA (ASFC) dhidi ya Biashara United raundi ya nne.
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Alhamisi, Januari 31 kwenye dimba la Taifa
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema kambi hiyo ya siku mbili itasaidia kuwaweka sawa wachezaji kabla ya kuwakabili Biashara United
Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo (kwenye ligi na SportPesa), Yanga itakuwa na nafasi ya kusahihisha makosa kwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo na kutinga raundi ya tano ambayo ni hatua ya 16 bora
Ratiba ya mabingwa hao wa kihistoria inaonyesha baada ya mchezo huo, wataelekea mkoani Tanga kuikabili Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa Jumapili, Februari 03 2019
No comments:
Post a Comment