We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, January 30, 2019

Video: Sugu aimwagia sifa Serikali Bungeni

Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema Joseph Mbilinyi, almaarufu Sugu, amekunwa na utendaji kazi wa wizara ya afya na kuimwagia sifa mbele ya Bunge. 


Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo bungeni Jumatano Januari 30, 2019 wakati akiuliza swali la nyongeza kufuatia swali lake la msingi alipotaka kujua kuhusu ukamilishaji wa jengo la maabara katika hospitali ya rufaa.



Sugu  amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumpeleka Mbeya balozi mteule Dk Mpoki Ulisubisya ili awe mkuu wa mkoa huo kwa madai kuwa ni hazina nzuri ambayo kuipeleka mbali ni kuondoa rasilimali muhimu kwa taifa.

 "Mnasema hatushukuru, naomba kuishukuru wizara hii kwa namna ilivyosimamia na kutengwa fedha Sh5 bilioni kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la maabara na ununuzi wa vipimo vya kisasa kama CT Scan na MRI," amesema Sugu na kuongeza

"...lakini ningekuwa na uwezo wa kumshauri Rais Magufuli ningemwambia badala ya kumpeleka ubalozi aliyekuwa katibu mkuu wizara ya Afya Dk Mpoki, basi angemleta kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya ili utaalamu wake ubaki hapa nchini badala ya kupoteza utaalamu wake na uwe mbali."

Msikilize hapo chini

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list