We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, January 29, 2019

Kama haupo kwenye kundi hili wewe ni muhujumu uchumi – RC Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaagiza wakuu wa Wilaya kuhakikisha hadi kufikia 01/03/2019 kila mfanyabiashara mdogomdogo anakuwa na Kitambulisho cha utambuzi kilichotolewa Na Rais Dkt. John Magufuli huku akiwataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo. 


RC Makonda akimkabidhi DC wa Mjema boksi la vitambulisho vya Machinga


RC Makonda amesema kuwa baada ya Tar 01/03/2019 mfanyabiashara yoyote atakaekutwa hana kitambulisho, leseni ya manispaa au vielelezo vya kukipa kodi TRA atajikuta mikononi mwa vyombo vya dola kama muhujumu Uchumi.
Mhe. Makonda ameyaeleza hayo leo wakati wa kikao na watendaji wote wa mkoa kilichoenda sambamba na kugawa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo kwa Wakuu wa Wilaya na kufanya mkoa huo kuwa kinara kwa kupokea takribani vitambulisho 175,0000 kutoka kwa Rais Magufuli.
Aidha RC Makonda amesema baada ya 01/03/2019 serikali ya mkoa itawaingiza wafanyabiashara hao katika mfumo wa kisasa (Database) utakaowezesha serikali kuwafikia na kuwapa mafunzo ya namna kukuza biashara zao ili mwisho wa siku wafikie uchumi wa Kati.
Pamoja na hayo RC Makonda amewatahadharisha watendaji wanaowatoza kiasi kikubwa cha fedha ya kitambulisho tofauti na bei elekezi ya Tsh 20,000 huku akiwahimiza wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo waliyopewa na Rais.
Mbali na Vitambulisho RC Makonda ametoa miezi miwili kwa Wakurugenzi wa Manispaa kuhakikisha Leseni za wafanyabiashara zinaingizwa katika mfumo mmoja ikiwa ni pamoja na kuharakisha utoaji wa leseni ili kupunguza usumbufu kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list