Spika wa Bunge, Job Ndugai amewatuliza wabunge wa CCM waliokuwa wakiomba mwongozo ili kupangua hoja za wapinzani kuhusu muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa.
Hayo yametokea jana Jumanne Januari 29, 2019 wakati mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe alipokuwa akichangia muswada huo bungeni jijini Dodoma.
Akiwajibu wabunge hao, Ndugai amesema kuwa kwa sababu ya muda waliamua tangu asubuhi kuwa hawataruhusu miongozo wala taarifa isipokuwa utaratibu unaotokana na kanuni kukiukwa.
No comments:
Post a Comment